Hatimae Ujenzi 'Flyover' za Ubungo wazinduliwa


Ujenzi wa barabara za juu (Flyover) katika makutano ya barabara ya Ubungo umezinduliwa leo mara baada ya Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim kuweka jiwe la msingi.

Barabara hizo za juu za ngazi tatu (Interchange), itagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 188.71 na itajengwa kwa muda wa miaka 3 na kuhusisha barabara za Nelson Mandela na Sam Nujoma ambapo takribani magari elfu 60 ambayo yatatumia barabara hizo kwa siku na kuwa mwarobaini wa msongamano wa magari katika makutano ya eneo la Ubungo.


Akihutubia katika uzinduzi huo, Rais Dkt. Magufuli amesema serikali yake inalenga kuboresha miundombinu ya barabara ili kurahisisha usafirishaji na kuchochea mapinduzi ya viwanda na kuweka wazi miradi mingi ya ujenzi wa barabara ambayo analenga kuijenga hivi karibuni na kuiweka Tanzania kwenye nchi ya uchumi wa kati.
Powered by Blogger.