Hatimae Nay ‘Asanda’ kwa Madee kisa hiki


Mkali asiyeishiwa vituko kunako Muziki wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kidizaini kama amelimaliza bifu ‘amesanda’ kwa hasimu wake, Hamad Ally ‘Madee’ baada ya kumfagilia kuwa ni miongoni mwa wasanii wachache wa Hip Hop wanaofanya vizuri kwa sasa.

Nay alidai licha ya kwamba Madee ni hasimu wake kimuziki lakini anakubali kazi za mwanamuziki huyo asiyechuja kwa kuwa anajua kusoma alama za nyakati.

“Ni msanii mzuri anajitahidi, anatoa ngoma kali, anajua kuandika vizuri na hata melodi zake ziko poa, kimsingi anajua kusoma alama za nyakati katika kila zama za muziki huu wa Bongo, nikipewa nafasi ya kumzungumzia Madee nafikiri hilo ndilo ninaloweza kusema,” alisema Nay wa Mitego kwenye Over Ze Weekend.
Powered by Blogger.