Harmonize: Sijui kama Jackline Wolper amewahi Kudate na Diamond Platnumz
Msanii wa muziki wa Kizazi Kipya Harmonize amesema kuwa yeye hafahamu
kama Diamond Platnumz alishawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na
Jackline Wolper ambaye ndie mpenzi wake kwa sasa.
Harmonize alisema hayo alipoulizwa katika kipindi cha The Playlist kama
anajisikia vibaya Kuwa na mahusiano na Mwanamke ambaye Boss wake
Diamond alishawahi kuhusishwa katika tetesi za kimapenzi pamoja nae.
“I dont know About that, sijui kama Jack alishawahi kudate na Chibu D, Sijui, Sijawahi kusikia” Alisema Harmonize
Harmonize aliendelea kusisitiza msimamo wake kwamba hakuwahi kusikia
popote habari za wawili hao kuwa na mahusiano ya kimapenzi hapo awali na
kusema kuwa kwake ni kitu kipya na ndio amekisikia kwa mara ya kwanza.
“Mimi mwanakijiji Bro, Mjini sijafika Siku nyingi, so sijui na
sijawahi kusikia, ndio kwanza Unanisuprize, Kumbe Ilishawahi kutokea
Hivyo?” Alihoji Harmonize.