Harmonize Ampa Saluti Korede Bello

 


Msanii wa Bongo Fleva anayetikisa na vibao vingi ikiwemo Matatizo na Bado, Rajab Abdulhan ‘Harmonize’ amemfungukia msanii kutoka Nigeria, Korede Bello kuwa amemfunza mengi alipokutana naye.

Harmonize alisema kuwa, Korede Bello anayebamba na Ngoma ya Do Like That ni moja kati ya wasanii ambao wataishika Afrika na dunia nzima soon kwa jinsi anavyomuona.

 

“Simsifii kwa kuwa nimekaa naye kwa muda na kufanikiwa kutengeneza naye ngoma, hapana! Korede ni mmoja kati ya wasanii wa kuangaliwa sana kwa mwaka huu.

Amenifunza mengi ikiwemo mbinu za kuliteka soko la Afrika. Kama utaona tayari ameshafanikiwa kufanya kolabo na watu wakubwa duniani akiwemo Kelly Rowland,” alisema Harmonize.
Powered by Blogger.