Harmonize Afatwa Na Difenda Za Polisi Akiwa South Africa

Hii imetokea nchini South Africa pale Harmonize na Wolper walipokwenda kurekodi video yake ya wimbo mpya wa Niambie, Njiani wakati warudi toka location usiku Harmo alimuudhi kidogo Wolper na Wolper akaamua kununa ili kuona kama Harmo atambembeleza kimahaba.

Basi pale walipofika getini ambako wamefikia mlinzi alichelewa kidogo kufungua mlango na Wolper ndipo alipogeuka nyuma na kufanya kama anarudi walikotoka huku akisema nataka kurudi nyumbani, ndipo hapo Harmo alipoamua kumfata na kumbembeleza huku mbwa wa maeneo hayo walikuwa wanabweka sana. Ghafla hapo hapo zikatokea gari za polisi kama tatu na kuwauliza nini kinaendelea. Msanii Harmonize akaamua bora kuwaongopea polisi kwa kusema "HUYU NI MPENZI WANGU NA MIMI NI MSANII WAKATI TUNARUDI NJIANI KATIKA SIMU YANGU ILIINGIA MESEJI NA MAPENZI KWAHIYO HAPA KAKASIRIKA NAJARIBU KUMBEMBELEZA TUINGIE NDANI"
Polisi ikabidi wachukue namba ya simu ya Harmo na Email yake kisha wakaruhusiwa kuingia ndani.
Powered by Blogger.