G Nako auza video hii Sh. 300
Mkali wa kurap Bongo,
George Mdemu ‘G Nako’ amefunguka kuwa baada ya kufanya biashara ya
kuuza nyimbo zake kwa muda mrefu katika mfumo wa audio mitandaoni sasa
ameingia rasmi kuziuza kwenye mfumo wa video ili kutanua soko la muziki
wake duniani.
Akichonga na Uwazi Showbiz, mkali huyo anayefanya poa na ngoma yake iitwayo Go Low aliyomshirikisha Jux huku
ikitengenezwa na Prodyuza Lua wa Switch Records alisema video zake zote
kwa sasa hazipatikani bure mitandaoni, bali zinapatikana kwa shilingi
300 tu.
“Tumefanya kazi za
bure muda mrefu sana, mashabiki wangu watakuwa wanaelewa wazi kuwa kwa
muda wote niliokuwa ninafanya kazi video
zangu zilikuwa zinapatikana bure mitandaoni, kwa hiyo kwa sasa nimeamua
kujiweka kibiashara zaidi na ninaimani nitafanikiwa zaidi,” alisema G
Nako.