Fid Q aanika ukweli kuhusu kwa nini hakumpa namba yake Edu BoyMkali Fid Q amesema kuwa alishindwa kumpa namba yake msanii Edu boy kwakua hakua anamfahamu sana kiasi cha kumuamini kumpa namba yake binfsi ya simu.

Fid amesema kuwa namba yake sio namba ya taifa kuwa sio kila mtu anaweza kuwa nayo bali ni baadhi ya watu anaowaamini na kuwafahamu vizuri ndio wanaoweza kuwa na namba yake na si vinginevyo.

“Sijajua kwa nini aliamua kuchukulia hivyo mimi nilishindwa kumpa namba yangu kwakua sikuwa namfahamu sana Edu boy kwa kipindi kile na namba yangu sio namba ya Taifa kuwa kila mtu awenayo na huwa nawazingua sana watu wanaotoa namba yangu kwa watu mabumashi”
Fid alikiambia kipindi cha the Playlist.

Inshu hii imekuja baada ya wimbo mpya wa Edu boy uliomchana kuwa alimnyima namba ya simu wakati wa hustle zake za kutoka.
Powered by Blogger.