Duu!! Nicki Minaj Ampiku Aretha Franklin Kama Msanii Wa Kike Mwenye Nyimbo Nyingi Kwenye Billboard Hot 100


Nicki Minaj amempiku mwanamuziki mkongwe, Aretha Franklin kama mwanamke mwenye hits nyingi zaidi kwenye Billboard Hot 100.

Mwezi huu Minaj aliingiza nyimbo tatu kwenye chati hiyo, ‘No Frauds’ akiwashirikisha Drake na Lil Wayne (No. 14), ‘Regret in Your Tears’ (No. 61) na ‘Changed It’ akimshirikisha Lil Wayne (No. 71). Kwa nyimbo hizo, sasa Minaj amekuwa na nyimbo 76 zilizoingia kwenye Hot 100 na kumpiku Franklin mwenye nyimbo 73.

Franklin alikuwa ameishika nafasi hiyo kwa takriban miaka 40. Hapo chini ni orodha ya wanamuziki wa kike wenye nyimbo nyingi katika chati hiyo kuanzia Aug. 4, 1958 hadi April 1:

76, Nicki Minaj
73, Aretha Franklin
70, Taylor Swift
58, Rihanna
57, Madonna
56, Dionne Warwick
54, Beyonce
53, Connie Francis
48, Mariah Carey
48, Brenda Lee
43, Miley Cyrus
41, Barbra Streisand
40, Mary J. Blige
40, Janet Jackson
40, Diana Ross

Powered by Blogger.