DUH! WACHEZAJI WA PSG WAPOKELEWA UWANJA WA NDEGE KWA MAWE


Klabu ya Paris St Germain ya nchini Ufaransa usiku wa jana kuamkia leo walipokelewa na mashabiki wao kwa kupopolewa na mawe.

Wachezaji hao walipata hadha hiyo ni baada ya kupata kipigo kikali cha kihistoria cha goli 6-1 kutoka kwa wababe wa nchini Hispania yani klabu ya Barcelona.

 Hiyo inatokana na mtanange wa kombe la klabu bingwa Ulaya mchezo wao kwanza wa PSG nakupata ushindi wa goli 4-0 katika dimba lake la nyumbani Parc Des Princes nchini Ufaransa na ndipo katika mchezo wa marudiano kupinduliwa kwa matokeo hayo katika dimba la Nou Camp nchini Hispania kwa wenyeji Barcelona kushinda kwa goli 6-1 na mchezo kumalizika kwa jumla ya magoli 6-5 matokeo yaliyopelekea kushangaza Dunia na kuwaudhi mashabiki wake na kupelekea kuwafanyia fujo katika Uwanja wa ndege kwa kuwapiga mawe na kuwavamia kwenye magari yao walipowasili nchini kwao.

Powered by Blogger.