Dkt. Kafumu, Vicky Kamata wajiuzulu nyadhifa za Bunge

 http://i0.wp.com/dar24.com/wp-content/uploads/2016/11/wabunge.1.jpg?resize=595%2C344
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Dkt. Peter Kafumu na Makamu wa Kamati hiyo, Vicky Kamata wamejiuzulu nafasi zao leo.  Wawili hao ambao ni wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wametangaza uamuzi huo kupitia barua waliomuandikia Spika wa Bunge hilo, Job Ndugai.

Dkt. Kafumu ni mbunge wa jimbo la Igunga tangu mwaka 2011, na Vicky Kamatta ni mbunge wa viti maalum mkoa wa Geita, wote kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi. Hata hivyo, katika barua hizo zilizosambazwa mitandaoni, hawakueleza sababu zilizopelekea kuchukua uamuzi wa kujiuzulu, bali wametoa shukurani kwa Spika wa Bunge pamoja na wajumbe wa kamati hiyo kwa ushirikiano wao.


 
 Dkt. Dalaly Peter Kafumu

“Nakushukuru sana kwa ushirikiano na uongozi ulionipa katika kuongoza Kamati hii nyeti,” inasomeka sehemu ya barua ya Dkt. Kafumu.
Powered by Blogger.