Diamond Platnumz: Sina Shida Yoyote Na Ali Kiba


Mmiliki wa Record Label ya Wasafi Classic Baby WCB Diamond Platinum amesema kuwa uongozi wa wasafi unafanya mazungumzo na Menejimenti ya Ali Kiba iliwaje kuuza muziki kwenye website aliyoizundua hivi karibuni ya wasafidotcom.

Diamond amesema kuwa hana tatizo lolote na Ali Kama watu wanavyozusha kwenye mitandao na baadhi ya vyombo vya habari vinavyo vumisha na ameshawahi kukutana na Ally Kiba mjini Nairobi na wakazungumza mambo kadhaa.


“Ali Kiba ni mtu ambaye tunaheshimiana naye nilimjua kupitia dada yangu Queen Darlin na tushawahi kukutana nchini Kenya tukazungumza juu ya kinachoendelea,na kwa sasa uongozi wangu anafanya mazungumzo na menejimenti yake ili waje kuuza muziki kwenye website ya wasafi.com”
Powered by Blogger.