Dayna Nyange Sio Single Girl, Kaziweka Wazi Sababu Za Kutomuanika "Bae" wake
Akizungumza katika Story tatu za Planet Bongo ya East Africa Radio, Dayna amesema kumuweka mpenzi wake katika mitandao ya kijamii kunaweza kumsababishia ugomvi wa kila siku katika mahusiano yake na kwamba anafurahia maisha ya usiri waliyojiwekea yeye na mpenzi wake.

"Kama anakupenda na kukuheshimu inatosha haina haja ya kum- 'post' katika mitandao ya kijamii, kwanza nikimuweka wazi mpenzi wangu nadhani ugomvi utakuwa hauishi ili kuepusha hayo mimi bora nimfiche, siku akija nyumbani nikamuwekea mkono akinivalisha pete mtaona kiwiliwili ila siku tukifunga pingu za maisha nitamuweka sura yake msijali", Amesema Dayna 

Dayna ameongeza kuwa katika jamii ya Tanzania mwanamke kuwa na mahusiano na wanaume zaidi ya watatu kabla ya kufikia ndoa ni uhuni tofauti na wanaume ambao wao huchukuliwa kama urijali.

"Kinachoniogopesha sana ni kwamba unaweza kujikuta wewe unampenda sana mwanaume kwa moyo wote alafu kumbe wewe moyoni mwake hata haupo, ukija kugundua hilo umeshachelewa na tayari umeshatangazia watu kwenye mitandao hapo ndipo watu wanaanza kukuhesabia ukionekana na mwingine tofauti na yule lazima wakuone muhuni hasa kwa sisi watu wenye majina ndiyo tabu zaidi. Ajue tu siwezi kum -post".
Powered by Blogger.