Breaking News: Magufuli ateua waziri mpya wa habari

 Rais Magufuli


Rais wa John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri na kumteua waziri mpya wa habari na michezo.

Katika Mabadiliko hayo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Palamagamba Aidan John Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

Aidha, Mhe. Dkt. Magufuli amemteua Dkt. Harrison George Mwakyembe kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. "Uteuzi huu unaanza mara moja," taarifa kutoka ikulu imesema.

Wateule wote wataapishwa Alhamisi kwa mujibu wa ikulu.
Powered by Blogger.