Arsenal Kukatwa Mishahara wakishindwa Kufuzu Champion League


Wachezaji wa Klabu ya Arsenal watakosa mamilioni ya Bonasi endapo watashindwa kufuzu katika michuano ya klabu bingwa Ulaya kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1997.

Imeripotiwa kuwa wachezaji wengi wa Arsenal katika mikataba yao kuna kipengele cha kupata bonusi kama watafuzu kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya.

Vijana hao wa Arsenal Wenger sasa wapo katika nafasi ya 5 kwenye msimamo wa ligi kuu , pointi 5 nyuma ya Liverpool ambao wa namba 4, huku wakiwa na michezo miwili mkononi.

Pia imeelezwa kuwa baadhi ya wachezaji wanaweza wakalazimishwa kukubali kupunguziwa mishahara (Pay Cuts) kama klabu hiyo haitafuzu michuano hiyo ya Ulaya.

Hii ni tofauti na klabu ya Chelsea ambao wao licha ya msimu uliopita kushindwa kufuzu kwenye michuano klabu bingwa Ulaya,waliendelea kuwalipa wachezaji wao mishahara ile ile. Wao wanatoa kipaumbele cha kuwalipa vizuri wachezaji kwa kushinda makombe kuliko kufuzu kwenye michuano ya Ulaya.

Timu kutoshiriki kwenye klabu bingwa Ulaya kunaikosesha mamilioni ya pesa. Msimu jana Arsenal ilipokea Pauni milioni 46.7 kutoka UEFA kwa kuingia hatua ya 16 Bora.
Liverpool walipokea kiasi cha pauni milioni 33.1 kwa kuingia fainali ya Europa Ligi ambapo walipoteza kwa Sevilla. Tottenham ambao pia walikuwepo kwenye michuano ya Europa Ligi walipokea kiasi cha pauni milioni 18.3.Powered by Blogger.