Agizo La Rais Magufuli Kuhusu Kampuni Ya Dangote Na Uchimbaji Makaa Ya MaweRais  John Magufuli ameagiza kampuni ya saruji ya Dangote kupewa ruhusa ya kuchimba makaa ya mawe nchini humo ili iweze kuutumia kwenye kiwanda chake kilicho mtwara kwa mujibu wa gazeti la The Citizen.
Dr Magufui aliliamrisha shirika la maendeleo ya taifa NDC kuipa kampuni hiyo sehemu ya mgodi wa mkaa wa mawe wa Ngaka ulio wilaya ya Mbinga.

 Rais Magufuli alitoa agizo hilo kabla ya kuzindua malori 580 ambayo yatatumiwa kusafirisha simiti kutoka kwenye kiwanda hadi sehemu tofauti za nchi.
Magufuli anasema anafahamua kuwa uzalishaji wa saruji kwenye kiwanda hicho umekuwa ukikumbwa changamoto kadha.

Aliongeza kuwa uchimbaji uliokuwa ukifanywa na kampuni ya Tancoal Energy Limited ulikuwa duni.

"Chini ya makubaliano ni vigumu kuhakikisha kuwa muwekezaji anapata makaa ya mawe ya kutosha kwa uzalishaji wa sarujii kwa sababu ya uzalishji mdogo wa makaa.

"Kwa hivyo mumpe Dangote kipande cha ardhi kwenye mgodi ili apate kuchimba makaa kwa matmizi ya kiwanda chake," alisema Rais Magufuli,

BBC
Powered by Blogger.