Achilia Mbali Zile Ngoma Na Makolabo Mfululizo, Hii Hapa Rekodi Nyingine Kutoka Kwa Future Mwezi HuuRapa Future ameendelea kukaa kwenye headlines za  burudani kwa muda mrefu sasa kufuatia kolabo za kutosha na ngoma zake binafsi ambazo rapa huyo amekua akiziachia mfululizo,
 Mwezi uliopita Future aliwatendea haki mashabiki zake baada ya kuachia albamu mbili ambazo zilipishana wiki mbili za kuingizwa sokoni.

Kwenye orodha ya albamu zinazofanya vizuri marekani wiki hii mnyamwezi Future amevunja rekodi kwa kushikilia nafasi ya kwanza na ya pili kupitia albamu zake "HNDRX na FUTURE" Future amethibitisha hayo kupitia ukurasa wake wa twitter.


Future ameshindwa kuzificha hisia zake na kuamua kuutumia ukurasa wake wa twitter kama sehemu ya kushukuru na kutoa ushawishi kwa mashabiki zake.
Licha ya kuwa na Albamu mbili sokoni ambazo zote zinafanya vizuri, Kutoka kwenye albamu yenye jina lake "FUture" ngoma "Draco" ndiyo homa ya mabishoo... Cheki nayo hapa chini:
Powered by Blogger.