Zari Kayasema Yote Asiyoyapenda Kwa Diamond Platnumz, Maelewano Na Mama Mond, Udaku Wa Mitandaoni Na Simu Za Mikononi

Leo kwenye Leo Tena ya Clouds FM kinachoruka kila siku za jumatatu mpaka Ijumaa kulikua na ugeni wa mbongoflava Diamond Platnumz na Babymama wake Zarithebosslady,

 Moja kati ya vitu wameongelea ni mahusiano yao na Arobaini ya mtoto wao wa pili Prince Nillan.

Akijibu swali la Dahuu (Mtangazaji wa kipindi hicho) lililouliza kama wawili hao wamewahi kugombana, Zari amesema kugombana ni lazima, kama kuna vitu vinatokea sivipendi au Diamond hapendi lazima kuzinguana, hatuwezi kwenda sawa siku zote.

Zari pia ameongeza yeye na Diamond wanashirikiana kila kitu isipokua simu za mikononi tu.

Kingine ambacho mwanama Zari amekitaja kutokupenda ni ishu ya udaku wa Instagram na mitandao mingine ya kijamii kwani siku za nyuma alikua akiamini sana katika udaku mpaka akagundua anatengeneza sumu mwilini mwake na kuhusu skendo za magazeti na kusema eti yeye na Mama Mondi haziivi ni uvumi tu kwani watu wanapenda kupandikiza matattizo sehemu ambazo hazina matatizo..

MSIKILIZE  HAPA:


Powered by Blogger.