Young Money Kuungana, Na Huu Ndio Ujio Mpya Wa Nicki Minaj Na DrakeUkiongelea makundi makubwa ya muziki yaliyowahi kuwa na rekodi nyingi duniani neno "Young Money: halitokosekana kwenye orodha yako right?

Sio tu neno "Young Money" litaifanya orodha yako kutimia, maana yake hakuana Young Money bila Drake, Nicki Minaj wala baba yao Lil Wayne au sio?,

Lilikua bonge moja la crew ambalo liliumiza sana miaka ya nyuma mpaka mara ya mwisho vichwa hivyo vitatu vinakutana kwenye ngoma "ONLY" ilikua ni hot kila kona.


Kuna msemo wa kiswahili "Vizuri Havidumu" huenda ikawa ni kweli kwani Young Money haikuweza kusurvive tena baada ya membaz wake kuanza kujiengua mmoja baada ya mwingine.

Ni Lil Wayne alianza kuondoka kwa kile alichodai ni kutetea maslahi yake, Drake nae akaanzisha Label yake "OVO SOUND" akishirikiana na prodyuza Noah Shabib..

Tupa kule mastori mastori ya kutengana, Young Money wanaungana tena, hayo yamesemwa na Drake kwenye moja ya Shows zake jijini London Uingereza.

Cheki Na Hii Video Hapa:


  

"Nimepokea simu kutoka kwa Nicki na amenituma kuwasalimia mashabiki zake, Hivyo mnajua lazima tufanye kitu kwa ajili ya muungano wa Young Money na mashabiki zake msimu huu" alisema Drake

Kwa mujibu wa Drake inaonekana Nicki na Drake wapo kwenye hatua zao za mwisho kabisa za kuachia kitu chao kipya, Tunajua balaa la hawa viumbe, Tuendelee kusubiri tuone wanakuja na nini baada ya kukaa tofauti kwa zaidi ya miaka miwili saa.
Powered by Blogger.