YANGA YAZIDI KUJIKITA KILELENI KWA KUICHAKAZA STAND UNITED

Wanajangwani hao wanazidi kujikita kileleni kwa kuwachapa timu ya Stand United kwa bao nne kwa bila yaani ni kasi ya 4G.
mchezo ulianza kwa kasi na ndipo yanga wakaanza kutikisa nyavu za chama la wana Stand United kupitia kwa Nyota wake Donald Ngoma akifuatiwa na mshambuliaji mwenzake Simon Msuva aliyefunga goli la pili dakika ya 26 nakuelekea mapumziko Yanga wakiwa wanaongoza kwa magoli mawili.
Katika kipindi cha pili yanga waliingia na moto wao uleule nakuwafanya wafunge goli jingine kupitia kwa nyota wake Obrey Chirwa nakumalizia msumari wa mwisho kutoka kwa nahodha wao Nadir Haroub Cannavaro. Ingawa pia yanga walikosa penati kupitia kwa mchezaji wake Simon msuva haikuhalibia furaha yao ya ushindi wa 4G
Kwa ushindi huo Yanga wanazidi kupasua anga kwa kujikita kileleni kwa pointi49 akimuacha nyuma mtani wake simba kwa pointi nne.
Powered by Blogger.