KOCHA AMBAYE ALICHUKUA KOMBE MSIMU ULIOPITA ATIMULIWA


Kocha ambaye alichukua kombe la ligi kuu ya nchini England msimu uliopita Claudio Ranieri amefutwa kazi.


Aliyekuwa kocha wa klabu ya Leicester city Claudio Ranieri (65) amefutwa kazi usiku wa kuamkia leo na waajiri wake klabu ya Leicester city.Kauli hiyo ilitolewa na makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo Mthailandi Aiyawatt Srivaddhanaprabha kuwa wanauheshimu mchango wake mkubwa katika klabu yao kwa kuwaletea kombe la ligi kuu na tunzo mbalimbali.
Kocha huyo raia wa nchini Italia kipindi anaitumikia klabu hiyo aliipatia pia na Tunzo mbalimbali kwa wachezaji kama Riyard Mahrez,Jamie Vardy,na yeye mwenyewe kupewa tuzo ya heshima pamoja na klabu.
Powered by Blogger.