WAKENYA WAZIDI KUNG'ARA KWENYE KILI MARATHON NA SIMANZI PIA IKITAWALA


Mbio za Kili Marathon zilishika kasi hapo jana Jumapili katika viwanja vya Gofu Moshi Club mkoani kilimanjaro zilizoshiriki nchi zaidi ya kumi na moja.

Kwenye mbio za Kili Marathon Wakenya wanazidi kuishikiria rekodi yao ya kuongoza kwa ushindi mkubwa  kwa kushinda katika mbio hizo zilizofanyika mkoani Kilimanjaro jijini Moshi nchini Tanzania ambapo mshindi wa nafasi ya kwanza hadi nafasi ya tano ni kutoka Kenya.
Na kwa upande wa Tanzania waking'ara katika Half Marathon mbio za nyika za Kilomita 21 kwa kushinda Over Roll Winner Mwanariadha Emannuel Giniki kutoka Manyara.

 Na kwa upande mwingine wa huzuni na simanzi ni baada ya kati ya wanariadha kutoka Kenya Mwanariadha Charles Maroa (36) kufariki Dunia katika mbio hizo hapo jana.Ilitokea ni baada ya kumalizika kwa mbio hizo alianguka chini ghafla na kupoteza Fahamu ndipo kukimbizwa Hospitali ya KCMC lakini alipofikishwa hospitalini hapo madaktari walibaini kuwa alishafariki.Powered by Blogger.