WAKENYA KUKIPIGA LEO NA HULL CITY YA ENGLAND


Leo katika Ulimwengu wa soka kutakua na mchezo mkali wa kirafiki kati ya KPL All Stars ya nchini Kenya dhidi ya Hull City ya nchini England.

Mchezo huo wa kirafiki ambao haujawahi kutokea wala Vilabu hivyo kukutana umeandaliwa na kampuni ya kubashiri(kubeti) michezo SportPesa unazikutanisha klabu ya ligi kuu ya England Hull City dhidi ya kombaini ya nyota wa ligi kuu ya nchini Kenya ambapo mtanange huo unachezwa katika Dimba la KCOM Stadium nchini Uingereza jiji la Kingston wenyeji wakiwa ni Hull City leo jumatatu majira ya saa tatu kamili usiku kwa saa za Afrika mashariki.
Mchezaji wa KPL All Stars Moses Odhiambo ambaye anachezea klabu ya Gor Mahia ya nchini Kenya akifanya Mazoezi katika nyasi za KCOM Stadium.


Powered by Blogger.