vijana wa serengeti boys watua bungeni.
Timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka (17)  pamoja na Rais wa Tanzania Foootball Federation wametembelea Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania hivi leo baada ya kupewa mwaliko na Spika wa Bunge kwa ajili ya kutambulishwa rasmi hapo bungeni kwa ajili ya mashindano waliyofuzu ikiwa pia ni pamoja na maandalizi ya kushiriki mashindano ya Afrika kwa vijana yatakayofanyika nchini Gabon mwezi wa nne.
 Na wabunge hao kukubaliana kuwachangia kwa kutoa posho zao.

Taarifa  za ujio wa serengeti boys mkoani Dodoma zilithibitishwa na Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Dodoma(Dorefa), Mlamu Nghambi.
Powered by Blogger.