Video: Harmorapa Ni Shida!! Leo kaja na hii mpya


Harmorapa ameonesha yeye sio mtu wa mchezo mchezo linapokuja suala zima la mtonyo, iko wazi hamorapa ni shida mjini.

Ikumbukwe kuwa Harmorapa ndiye msanii pekee aliyeweza kupata publicity kubwa ndani ya muda mfupi. Nini hasa kinachomfanya atrend na awe kwenye midomo ya watu? Muziki wake? Hapana, I bet asilimia 80 ya watu wanaomshangilia hawajui hata wimbo wake unafananaje, sababu hadi sasa video yake ingekuwa na zaidi ya views milioni 1. Kwahiyo, nini hasa story yake? Kwanini anaongelewa sana?  

Umaarufu wake umezungukwa na dhihaka na utani mwingi. Na hata jina lake lina maana ya kuwa yeye ni Harmonize anayerap. Kwa muda mfupi watu wakaanza kumfuatilia na kwakuwa binadamu hupenda vitu kama hivi – mzaha, jina lake likasambaa haraka na focus ikahamia kwake, kuliko hata Harmonize mwenyewe. Naamini hadi sasa wapo watu wanaomfahamu zaidi yeye kuliko hata Harmonize.

Leo kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmorapa ameamua kuonesha yeye ni mwamba kwa kupost clip fupi inayomuonesha akichezea dola.. 

Mbali na hilo msanii huyo Amekuja kupata kiki zaidi baada ya dancer wa Diamond, Mose Iyobo kumfananisha na nyani. Hapo, akaanza kupokea ‘public sympathy’ (huruma ya umma), ambayo inazidi kumpaisha zaidi.

Enjoy hapa na Video hiyo..


Powered by Blogger.