Video 8 Za BenPol Zitazokufanya Umkumbuke Mtu Valentine Hii:


Anaitwa Benard Paul, maarufu Kama BenPol na kuna jina limeongezeka siku hizi pia anaitwa "Bba Mali" Leo naamua kukusogezea nyimbo kadhaa za mshikaji zenye stori za mapenzi,
Nyimbo ambazo katika hali ya kawaida tu matukio kama haya yaliyopo humu ndani tunakutana nayo kwenye maisha yetu ya kila siku.

sina uhakika zaidi harakati zake zilianza lini lakini wengi tulipata nafasi ya kumjua mwaka 2010   baada ya kuachia "Nikikupata" wimbo ambao uliteka hisia za watoto wazuri wengi na kumfanya Ben kuwa mwanamuziki wa kiume anaependwa zaidi na watoto wa kike:

Cheki Hapa  Video Ya Nikikupata:

BenPol hakuridhika na mafanikio aliyopata kwenye "Nikikupata" nguvu aliyopewa na mashabiki wake wa kwanza kabisa aliingezea kwenye ujio wake mpya, Kwenye ngoma iliyofuata inaonyesha Ben Pol ameshampata mtoto mzuri na alikua anampa maneno fulani hivi ya kuzidi kumteka mtoto asahau shida zote za duniani. Rekodi nyingine ya Ben Pol ilikua inaitwa "Samboira". Cheki Na Video Yake Hapa:
Mapenzi na Samboira yalikua hot kinomanoma lakini yalikuja kuingia doa baada ya BenPol kupata umaarufu, Namba ya mashabiki iliongezeka kama nilivyokuambia hapo juu Ben ni mwanamuziki ambae style yake ya uimbaji inapendwa zaidi na watoto wa kike basi kuna shabiki wa kike alitaka kuvunja Penzi la Ben na Samboira baada ya kujiweka karibu na BenPol kwa kigezo anapenda uimbaji wa Ben na angetamani kujifunza kumbe alitaka penzi la mshikaji, Ni kwenye wimbo "Number One Fan" ndiko unaweza kukutana na story hiyo. Jikumbushe Na Hii Video Yake Hapa: Mrembo aliona kama Ben hasomneki akaamua kumchana tu baada ya kugundua mshikaji alikua anatoka na michepuko yake kimyakimya, ilikua ni tatizo kwa benpol na moyo wake ikabdi amwambie mtoto mzuri "Yatakwisha" Video ya wimbo huu haikuwahi kutoka japo ulikua wimbo mzuri pamoja na kuvuja lakini ulifanikiwa kufanya vizuri kiasi kwa mwaka 2013.

Baada ya hapo BenPol aliachia hits nyingine kadhaa mpaka alipoungana na mwamba wa Kaskazini mweusi JohMakini na kutengeneza kitu kinaitwa "Unanichora"


Hata mimi ukiniuliza stori ya "Samboira" iliishia wapi siwezi kukujibu baada ya muda mrefu hatimaye mshikaji alimwagana na mtoto "Samboira" na kuzama kwenye penzi la Baby mpya "Sophia" Penzi la Sophia lilimkoleza BenPol mpaka akaamua kumpeleka nyumbani kwao Dodoma..

 Cheki Hapa Ilivyokua:

Mwaka 2016 ulikua mzuri kwa BenPol aliamua kufungukia penzi lake kwa mtoto sijui kama ni Sophia au mwingine lakini kwenye moyo mashine Ben alikua akijaribu kumuweka sawa mtoto jinsi ambavyo jamaa anapenda mpaka haelewi, huenda huu ndio ukawa wimbo mkubwa kuliko zote ambazo BenPol aliwahi kufanya,Hajawahi kukosea kwani kwa kufungua mwaka 2017 Benpol ameachia "Phone" aliyompa shavu Mghana Mr Eazi, Kwenye ngoma hii kuna BenPol wawili yaani BenPol yule wa rnb yake tuliyizoea na hii style ambayo BenPol ameitumia kufanya Chorus ndio inafanya nikuambie kuna Ben Pol wawili, Kwa mtazamo wangu Hii nayo inaweka rekodi ya kuwa miongoni mwa nyimbo kali za RnB kuwahi kufanyika Tanzania na Afrika kwa ujumla. Kama Bado Haujaona Video Ya "Phone" Cheki Nayo Hapa:

Katika hizi video 8 nilizokuwekea hapo nina imani ipo moja kaau zaidi ambazo zitakua zimekukumbusha kitu kwenye maisha yako ya mahusiano, Ulikosea au ulikosewa?, Ulichukua hatua gani, Kusamehe au kusepa?,. Ulishawahi kumwambia mp[enzi wako/au alishawahi kukuambia kitu ambacho unahisi hautakaa usahau? Unawza Kutuachia Comment zako hapa chini Baadae turuke nazo.
Powered by Blogger.