UWANJA WA TAIFA KUTOA SULUHISHO LA SIMBA NA YANGA


Hakika Uwanja wa Taifa utatoa uamuzi katika pambano la watani wa jadi baada ya tambo za muda mrefu walizokua wanatambiana.

Katika mchezo huo uliobeba hisia za mashabiki wa klabu ya Yanga Wanawajangwani  na wa Simba wamsimbazi na watu mbalimbali na wengi wa nchini Tanzania na mipaka yake haswahaswa jijini Dar-es-salaam ambako unachezeka mchezo huo ambapo matokeo yake yanaamuliwa Uwanjani kuanzia majira ya saa 10:00.
Mchezo huo kwenye mzunguko wa kwanza klabu hizo zilitoka sare pacha ya goli moja kwa moja ambapo mtanange huo ulileta fujo uwanjani kwa mashabiki kung'oa viti vya uwanjani kwa kudai refa alitoa maamuzi ya ovyo kwa kukubali goli lililofungwa na mshambuliaji wa Yanga Amissi Tambwe kuwa silo la kihalali na kutoa kadi nyekundu kwa nahodha wao ambaye ni Jonas .E.  Mkude na kupinga maamuzi yake kwa hasira kali hiyo iliyopelekea kutokea hivyo.
Sasa tungojee matokeo katika mchezo huo utakuaje kwa wakongwe hao na watani wa jadi wa muda mrefu.
Powered by Blogger.