USIKU WA KLABU BINGWA ULAYA (UEFA) UKO HIVI LEO


Usiku wa klabu bingwa leo uko hivi baada ya vilio vya huzuni  na vicheko vya furaha vya jana usiku.

Real Madrid watakua nyumbani kwao nchini hispania katika dimba lao la kujidai Santiago Bernabeu wakiikaribisha klabu ya Napoli ya nchini Italia.
Huku klabu ya Real madrid wakiwa na nafasi kubwa ya kushinda kutokana na kuwepo nyumbani na kuwa karibu na mashabiki wao kwa wingi na endapo watatumia vyema uwanja wao huo wa nyumbani kwa kucheza soka la kujiamini na kuzitumia nafasi watakazozipata wanaweza wakatoka na ushindi.

Napoli nao sio wakuwabeza nao wako vizuri kwa upande wao kwa kucheza soka la umoja na kuongozwa na kapteni wao Marek Hamsik ambaye ni raia wa Slovakia anayecheza nafasi ya kiungo ni mbunifu na msumbufu sana kwa upande wa mabeki wa upinzani.


Kwa upande mwingine wa pili wa shilingi ni mchezo kati ya vijana wa Mzee Arsene Wenger yani Arsenal wa jijini london nchini uingereza na Bayern munich ya Carlo Ancelotti utakaopigwa katika dimba la Allianz Arena jijini munich nchini Ujerumani wenyeji wakiwa ni Bayern Munich wakiwakaribisha Arsenal.

Powered by Blogger.