umemsikia jamhuri kihwelu "julio" anavyosemaAliyekuwa kocha wa klabu ya mwadui Jamhuri kihwelu julio al maarufu wakujiita Perreira ameshangaza watu wengi hasa wa jijini la Dar es salaam kwa kutaka nyadhifa kubwa pale msimbazi.

kocha huyo mwenye maneno mengi na mbwembwe za kutosha alikuwa akiifundisha timu ya mwadui ya shinyanga kabla ya kuachana nayo kuna kipindi alizua gumzo baada ya kusema anaachana kabisa na masuala ya soka nchini Tanzania na kubaki kama shabiki tu kwa kuwa alizishwi na mfumo wa uchezeshaji wa waamuzi wa ligi kuu bara na kumpelekea kuachana kuachana kabisa na masuala ya soka nchini.
Lakini kocha huyo alikuwa akionekana katika baadhi ya mechi za mnyama yani Simba katika baadhi ya mechi kama simba ilivyocheza na majimaji jijini Songea kwa kuonwa na mashabiki na watu mbalimbali katika mechi zinazo muhusu mnyama na watu kushangazwa kwanini asiende kuangalia mechi ambazo timu yake aliyoiacha mwadui inavyocheza dhidi ya timu pinzani ila ni simba.

Kumbe kocha huyo ameibukia pale msimbazi klabuni simba na sasa ameibua hoja baada ya kujipigia chapuo katika nyadhifa ya maana pale msimbazi klabuni simba


      "Julio amesema kuwa kwa upande wake hana wasiwasi endapo viongozi wa simba wakiongozwa na rais wake Evans Aveva wakiamua kumpa nafasi hiyo kwani anaamini ana uwezo wa kuongoza .
"Siyo kama najipigia chapuo lakini kama viongozi wa simba wakiamua kunipa nafasi ya ukatibu sitaweza kukataa kwa sababu naipenda timu hiyo na kila mtu anajua na kama nikiwepo naamini nitaongeza kitu fulani na kuifanya timu ipate matokeo mazuri.
Uzuri wangu ni kwamba sikufungiwa na mtu yeyote kujihusisha na soka hivyo hata nikirejea hakuna ambaye atashtuka na niwaahidi kwamba nitaitumikia nafasi hiyo kuleta mabadiliko yaliyoshindikana kwa kipindi kirefu, "alisema julio.
katika nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Patrick Kahemele aliyerudi Azam.
Powered by Blogger.