Trump Apinga Amri Hii Ya Mahakama, Akata Rufaa

 
Serikali ya Marekani imewasilisha rufaa ya kutaka kurejeshwa kwa amri ya Rais Donald Trump ya kuwazuia raia wa mataifa 7 ya waislamu kusafiri hadi Marekani.

Hatua hiyo ya ni baada ya mahakama kuipinga hapo awali uwamuzi huo wa Rais Trump wa kuzuia baadhi ya mataifa kuingia Marekani.

Trump ameeleza kumpinga jaji aliyetoa uamuzi huo wa Mahakama, huku akionya kuwa watu wabaya na hatari, huenda wakamiminika hadi Marekani kutokana na uamuzi huo.

Kufuatia uwamuzi wa Trump kumekuwepo na maandamano dhidi yake huko Washington, jimbo la Miami na miji mingine kadhaa ya Marekani, pamoja na miji mingine mikuu ya bara Ulaya.
Powered by Blogger.