TID akiri wazi jambo hili juu ya suala zima la madawa ya kulevya


Msanii wa Bongo Fleva TID amekiri wazi kuwa alishawahi kutumia Madawa ya kulevya mbele ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo wakati akitaja majina ya watuhumiwa wa Madawa ya kulevya awamu ya Tatu.

TID amesema Madawa ya Kulevya yalimpeleka pabaya kwani familia yake iliyumba hata kiuchumi na hivyo ameamua kuunga mkono juhudi za RC Makonda kutokomeza madawa ya Kulevya.Mtazame hapa chini akifungunguka zaidi.

Awali TID alikamatwa na Wasanii wenzake watano kwa tuhuma za kujihusisha na Madawa ya Kulevya kabla ya kuachiwa kwa dhamana wiki iliyopita.
Powered by Blogger.