Tanzia: Kiongozi wa upinzani DRC Etienne Tshisekedi afariki dunia

 Tshisekedi alikuwa kiongozi maarufu wa upinzani kwa miongo kadhaa
Kiongozi wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Etienne Tshisekedi, amefariki dunia mjini Brussels nchini Ubelgiji akiwa na umri wa miaka 84.

Tshisekedi alikwenda mjini Brussels mwishoni mwa mwezi jana kwa ajili ya matibabu. Bwana Tshisekedi alikuwa mmoja wa wanasiasa wakongwe waliokuwa mstari wa mbele kupigania demokrasia ya nchi yake.

 Tshisekedi alikuwa na mvuto mkubwa kwa wananchi wa DRC

Alisimama kidete katika utawala wa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Rais Mobutu Sese Seko, ambae utawala wake ulidumu kwa miongo kadhaa kabla ya kupinduliwa.

Etienne Tshisekedi pia alikuwa mpinzani wa Rais Laurent Kabila, ambae aliingia madarakani mnamo mwaka 1997, na mwanae, Rais Joseph Kabila, ambae hivi sasa ndio anatawala nchi hiyo.


Je, Etienne Tshisekedi ni nani?


Akiwa mzaliwa katika jimbo la kati la Kasai mnamo mwezi Disemba mwaka 1932, bw Tshisekedi akiwa na umri wa miaka 79 alikuwa kiongozi wa upinzani mwenye umri mkubwa.

Alisomea sheria chini ya ukoloni nchini Ubelgiji. Harakati zake za kisiasa zilianza wakati wa uhuru wa taifa hilo mwaka 1960 ambapo alikabidhiwa nyadhfa za juu katika serikali ya kati mbali na utawala wa Kasaian uliokuwa mfupi.

Mnamo terehe 14 mwezi Novemba 2011, akiwa waziri wakati wa serikali ya dikteta Mobutu Sese Seko bw Tshisekedi alijimwaga katika siasa za upinzani 1980 wakati Mobutu alipoamua kufutilia mbali uchaguzi wote.
Akiwa kiongozi wa chama cha muungano wa Demokrasia pamoja na chama cha Social Progrees, amekuwa mpinzani wa serikali zote tangu wakati huo.

Wakati Mobutu alipolazimishwa kutengeza serikali ya muungano na upinzani, bw Tshisekedi alikuwa waziri mkuu mara mbili katika kipindi cha miaka miwili. Alijiuzulu nyakati zote hizo alipokosana na Mobutu.

Chama cha Bw Tshisekedi hakikushiriki katika vita wakati wa vita vilivyozuka baada ya utawala wa Mobutu kuanguka 1997, na hivyobasi kupata umaarufu mkubwa kutoka kwa raia walioathirika na mapigano hayo.

Baada ya kususia uchaguzi mwaka 2006, ambao anadai ulifanyiwa udanganyifu ,bw Tshisekedi aliamua kujitokeza na kuhakikisha kuwa anashinda.

-BBC
Powered by Blogger.