Songa Afunguka Kuhusu Mapokezi Aliyoyapata Kwenye Nyimbo Yake 'Mwendo Tu'Msanii wa muziki wa hip hop, Songa amedai hajawahi kupata mapokezi mazuri kwenye nyimbo zake kama aliyoyapata kwenye wimbo wake mpya Mwendo alimshirikisha Jay Moe.

Rapper huyo ambaye pia ni member wa Tamaduni Music, amedai video ya wimbo huo imekuwa ni video yake ya kwanza kuwa na views wengi kwa muda mchache.

“Kwa muda mfupi toka video itoke imeonyesha utofauti mkubwa sana katika muziki wangu, ni video yangu ya kwanza imeangaliwa zaidi YouTube kwa muda mchache. Pia ni wimbo ambao umeleta impact kubwa sana kwenye muziki wangu,” Songa aliiambia Planet Bongo.Katika hatua nyingine rapper huyo amedai kuna watu wengine wanamwambia kwamba amebadilika.

“Watu sasa hivi wanasubiri ngoma mpya ili kuona kama ndo nimebadilika kabisa au nimegusa tu huku,” alisema Songa.
Powered by Blogger.