SIMBA YATINGA ROBO FAINALI MBELE YA AFRICAN LYON

Jana katika Uwanja wa Taifa wa jijini Dar-es-Salaam kulikua na mtanange kati ya Mnyama Simba dhidi ya African Lyon.

Klabu hizo zote za kutoka jijini Dar es Salaam zilicheza mchezo wa kombe la FA (Azam Confederetion Cup) nakutoshana nguvu kwa Simba kushinda kwa goli moja kwa bila goli likifungwa na mshambuliaji wake wa kigeni kutoka Burundi Laudit Mavugo aliyefunga dakika ya 57 akipokea mpira safi kutoka kwa beki wa pembeni Mohammed Hussein "Zimbwe jr"na kisha kuuzamisha nyavuni.
Goli hilo la Simba linawavushwa kutoka hatua ya kumi na sita bora hadi hatua ya robo fainali katka kombe hilo.

Kikosi cha Simba; Daniel Agyei, Janvier Bukungu, Mohammed Hussein, Abdi Banda, Novalty Lufunga, James Kotei,Jonas Mkude, Said Ndemla, Laudit Mavugo, Juma liuzio.

 Kikosi cha African Lyon Rostand Youthe, Miraji Adam, Omaru Salum, Hamadi Waziri, Hassan Isiaka, Peter Mwalianza,Baraka Jaffary, Hamad Manzi, Rehani kibingu, Venance Joseph, Omary Data.


Powered by Blogger.