REAL MADRID YAGAWA KIPIGO NYUMBANI KWAKE


Real Madrid wazidi kupeta katika uwanja wake wa nyumbani kwa kugawa kipigo jana usiku dhidi ya klabu ya Napoli.

Ni usiku uleule wa ligi ya Mabingwa uliopamba kila kona ya macho ya wapenda soka  kwa kutazama mitanange mikali kama Bayern Munich dhidi ya Arsenal nchini Ujerumani na huku upande wa nchini Hispania ulikuwa mchezo kati ya wenyeji Real Madrid dhidi ya Napoli wa nchini Italia katika dimba la Santiago Bernabeu nchini hispania.
Katika mtanange huo uliotawaliwa na kadi nyingi za njano zilizotolewa na refa kwa Timu zote mbili na kucheza mchezo wa kuviziana kwa kila timu kujihami dhidi ya mwenzake ndipo klabu ya Napoli kuanza kwa kufunga goli la kwanza katika dakika ya nane kupitia kwa mshambuliaji wake Lorenzo Insigne raia wa nchini Italia nakuwa wanaongoza hadi dakika ya 19 matokeo yalibadilika baada ya mchezaji Real Madrid raia wa Ufaransa Karim Benzema kufunga goli kwa kupiga kichwa kilichozama mojamoja nyavuni nakwenda mapumziko wakiwa wote sawa kwa magoli kila Timu.
Kurudi kutoka mapumziko kwenye dakika ya 49 kiungo wa Real Madrid Toni Kroos aliifungia timu yake goli la pili akipokea pasi kutoka kwa mchezaji mwenzake Cristiano Ronaldo ambaye yeye kwenye mchezo kwa jana akupata bahati ya kushinda goli kunako dakika ya 54 kiungo wa Real Madrid Carlos Casemiro alifunga pazia la magoli kwa kupiga shuti kali lililozaa goli la tatu na kulipeleka mpaka mwisho wa mchezo kwa goli tatu kwa moja hadi mwisho wa mchezo huo.


Powered by Blogger.