Q Chillah Kundi Moja na Akina Harmonize… How Comes?

Najaribu kumfikiria Aboubakar Shaban Katwila wengi wamezoea kumuita Q Chief ama Q Chillah kuanzia mwaka 2008 enzi hizo akilikamata vilivyo soko la Muziki wa Bongo Fleva sambamba na wakali wengine aliotamba nao kipindi hicho kama Bushoke, Hussein Machozi, MB Dog na wengine wengi.

Uwezo wa kucheza na sauti ndivyo vitu vilivyowavutia wengi katika nyimbo zake, kama umepata bahati ya kusikia vibao vyake Si Ulinikataa, Wiper, Zaidi ya Jana, Ninachokipata, Mariam, Nikilala Naota, Uhali Gani naTutaonana Wabaya utaelewa namaanisha nini.

Mbali na vyote hivyo, nyota yake ilikuja kuzimika ghafla baada ya kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya ambapo alikuja kuibuka na kukiri kuwa alikuwa muathirika wa madawa hayo kwa zaidi ya miaka miwili na ameamua kuacha.

Lebo ya QS Mhonda Entertainment ilichukuwa jukumu la kumsimamia kazi zake akiwa pamoja na mkongwe mwenzake, MB Dog lakini baada ya kutoa ngoma nyingi kama vile Ganda la Ndizi, Sungura na Koku akimshirikisha staa wa Nigeria, Patoranking kulitokea kutokuelewana na lebo hiyo kwa madai amefanya nayo kazi kwa kipindi kirefu bila mafanikio.

Kwa sasa staa huyo hana lebo, kulikuwa na tetesi kwa muda mrefu kuwa anaweza kujiunga na Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) lakini hivi karibuni kiongozi wa lebo hiyo, Diamond alithibitisha kujipanga kumrudisha Q Chillah kwenye ramani ya muziki. 

Najaribu kuangalia muungano wa wasanii na taratibu zilizopo endapo atajiunga nao kwenye lebo hiyo ya WCB yenye wasanii wanne hadi sasa ambao ni Harmonize, Rayvanny, Queen Darleen na Rich Mavoko.

Ukongwe Kama nilivyoeleza hapo juu, Q Chillah ni mkongwe katika muziki huu, si mtu wa kupangwa foleni ya kusubiri f’lan atoke kwanza ndiyo afuate yeye japo wasanii hao nao ni wakal.

Credit: Ijumaa|showbiz

Powered by Blogger.