PSG NA BENIFICA WALALA USINGIZI MZURI BAADA YA USIKU WA JANA KUGAWA DOZISiku ya jana majira ya usiku ulikuwa ni usiku wa mabingwa kukutana katika viwanja mbalimbali na nchi tofauti za ulaya.

Katika dimba la Parc des Paris ya Paris nchini Ufaransa wenyeji wakiwa ni PSG-Paris Saint Germain wakiwapa dozi nene wageni wao Barcelona kwa kipigo kikali cha 4G kwa bila.
Magoli yakiwekwa wavuni na mshambuliaji Angel De Maria raia wa Argentina aliyeanza kufunga kwa faulo iliyozama moja kwa moja golini na goli la pili likiwekwa wavuni na mshambuliaji raia wa Ujerumani Julian Draxler aliyetua klabuni hapo akitokea klabu ya Wolfsburg ya nchini kwao na goli la tatu kuwekwa tena wavuni na yuleyule muargentina Angel deMaria na kumalizia la nne kwa  kuwekwa kimiyani na mshambuliaji Edinson Cavani nakugongelea msumari wa mwisho.


 


 
Huku kwa upande wa Benfica wakitoa dozi kwa Borussia Dortmund kwa goli moja kutoka kwa mshambuliaji wake mugiriki Konstantinos Mitroglou kwakufunga goli lililotokana na kona dakika ya 47 na ndani ya dakika 57 mchezaji wa raia wa Gabon Pierre Emerick Aubameyang kukosa penati waliyopata hadi mwisho wa mchezo unamalizika kwa goli moja hilo.
Powered by Blogger.