Picha: Bosi wa Sea Cliff na Hussein Pambakali walivyowasili central Ijumaa hii

 
Watu 65 waliotuhumiwa kuhusika kwenye sakata la biashara ya Madawa ya kulevya na kutakiwa kuripoti Ijumaa hii central polisi kwajili ya upepelelezi, baadhi yao wameitikia wito huo huku wengine wakishindwa kuitikiwa wito huo.

Hivi karibuni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda aliyaanika majina wa watu 65 ambao wanatuhumiwa kujihusisha na biashara ya Madawa ya kulevya na kuwataka kuripoti kituoni hapo ijumaa hii.

Kamera ya Bongo5 iliwashuhudia watuhumiwa watatu maarufu ambao ndio waliofika kituoni hapo akiwemo mbunge wa zamani wa Kinondoni, Iddi Azzan, Hussein Pambakali na mmiliki wa hoteli ya Sea Cliff.

Wakati huo huo mfanyabiashara maarufu Yusuph manji na askofu Josephat Gwajima waliowasili kituoni hapo siku ya Alhamisi lakini bado wanashikiliwa na jeshi hilo la polisi kwaajili ya mahojiano zaidi.

Naye mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ndiye aliyekuwa akisubiriwa kwa hamu na wafuasi wake wengi waliokuwepo kituoni hapo hakuweza kuwasili kituoni hapo.

Tazama picha hapa chini za Hussein Pambakali na mmiliki wa hoteli ya Sea Cliff wakiwasili kituo cha kati cha polisi.

Hizi hapa picha hizo
 Hussein Pambakali aliyevaa kanzu (damu ya mzee) akiwasili kituo cha polisi cha kati na mwanasheria wake

 

 

 

Mmiliki wa hotel ya Sea Cliff akiwasili polisi

  


Picha: credit Bongo5 
Powered by Blogger.