Nandy Afunguka Kilichokwamisha Video Ya 'One Day' Kuchelewa Kutoka


Hit maker wa 'Nagusagusa' Nandy ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya 'One day' amefunguka juu ya kuchelewa kutoka kwa video hiyo.

Nandy alidai kuwa anapokea sana request za mashabiki zake wakihitaji video lakini alishindwa kufanya kwa wakati sababu alilazwa kwa matatizo ya vidonda vya tumbo.
"Unajua wimbo wangu wa One day umetoka kama wiki kadhaa hivyo nimekuwa napokea request nyingi kutoka kwa mashabiki wakitaka video, lakini tumshukuru Mungu hata leo nipo hapa maana kama wiki moja hivi nilikuwa siwezi kuamka hata kitandani nilikuwa nasumbuliwa na 'Stomach ulcers' hivyo nilishindwa kufanya hata vitu vyangu binafsi ili nawaahidi kuanzia sasa muda wowote video ya One day itatoka" alisema Nandy kwenye FNL.
Powered by Blogger.