muizraieli wa ghana abwaga manyanga


Aliyekua kocha wa timu ya Taifa ya ghana raia wa izraeli Avram Grant ametangaza kuacha kuifundisha timu hiyo ya Ghana.

Kocha huyo aliyekuwa anaifundisha timu hiyo ya Black stars tangia mwaka 2012 tarehe 14\5 ndipo alianza kukinoa kikosi hicho akitokea klabu ya nchini Sebia Partizan Belgrad aliyetoka kuwapa ubingwa wa ligi ya  nchini hiyo na kuhamia timu ya taifa ya Ghana kipindi hicho nakuwapa mafanikio mengi kama kuwafuzisha ghana kwenye fainali za kombe la Dunia la mwaka 2014 kwa upande mwingine wa Afrika amewafikisha katika hatua ya fainali za Afcon mwaka 2015 ingawa hawakuchukua kombe mbele ya ivori coast.
Sasa kocha huyo ametangaza kuachia ngazi katika timu hiyo kwa sababu ya kutoka kwenye nusu fainali za afcon mwaka huu 2017 kwa kupewa kipigo na mabigwa wa sasa wa Afcon yaani Cameroon kwa magoli mawili kwa bila na pia kwenye ushindi wa tatu kukosa kabisa mbele ya Burkina Faso kwa kipigo cha goli  moja nakumpelekea kocha huyo kuchukua maamuzi hayo yaliyotokana na kutotimia malengo yake ya kuchukua kombe hilo.
na ikumbukwe pia kocha huyu ndiye aliyepokea mikoba ya jose mourinho pale klabuni chelsea kwa msimu mmoja mwaka 2007-2008 na pia aliifundisha west ham ya uingereza 2010 hadi 2011.


Powered by Blogger.