MATOKEO YA USIKU WA KLABU BINGWA KWA JANA HAYA HAPA


Wababe wa Italia watamba kwenye klabu bingwa ulaya kwa kutoa kichapo ugenini nchini Ureno.

Klabu ya Juventus ya nchini Italia imeendelea kugawa dozi hadi ugenini kwa kichapa klabu ya Fc Porto ya nchini Ureno kwa kipigo cha bao mbili kwa bila kutoka kwa winga wake Marko Pjaca dakika 72  na kwenye dakika ya 74 beki wake upande wa kulia Dani Alves akiiandikia kalamu ya mwisho ya magoli.
Na kwa upande wa pili wa kalata nchini Hispania wenyeji Klabu ya Sevilla waliwatandika klabu ya Leceister city kwa kipigo cha goli mbili kwa moja magoli ya Sevilla yalifungwa na kiungo Pablo Sarabia dakika 25 na kwenye dakika ya 62 kiungo wake Joaquin Correa na kwa upande wa klabu wa Leicester city yakifungwa na mshambuliaji wake Jamie Vardy baada ya kipindi kirefu sawa na dakika 748.

Powered by Blogger.