Kupitia "Marry You" Aliyomshirikisha "Ne-Yo" @DiamondPlatnumz Yupo Kwenye Rekodi HiiNi Februari 18,2017 siku ambayo video "Marry You" ya mbongofleva Diamond Platnumz imetimiza siku 16 tangu tarehe 02/02/2017 ilipondishwa kwenye mtandao wa youtube,
 Licha ya kukaa zaidi ya wiki mbili mtandaoni Video hii imeendelea kukaa kwenye orodha ya zile video kumi za bongoflava ambazo zinaendelea kufanya vizuri mtandaoni.

Tunafahanu kama Diamond Platnumz ameingia mkataba na "Universal Music Group" ambao wamempatia Diamond Chaneli mpya ya Youtube inayomilikiwa na mtandao wa "Vevo", Licha ya kuwa na Chaneli mpya kwenye mtandao wa youtube, Diamond Platnumz ameendelea kuishikilia rekodi yake ya kuwa msanii wa Bongo ambae video zake zinaongoza kwa kuangaliwa kwenye mtandao wa Youtube.

Marry You ambayo Mtanzania Diamond amemshirikisha Mmarekani Ne-Yo inashika nafasi ya 9 kati ya zile video zinzoangaliwa mara nyingi "YouTube" . Mpaka sasa video hiyo imetazamwa zaidi ya mara milioni 3 ndani ya wiki mbili tu.

Kama Ulikua Haujaiona Unaweza Kucheki Nayo Hapa:
Powered by Blogger.