MANCHESTER UNITED YAN'GAA EUROPA HUKU WAKINA SAMATTA WAKITOKA SARE

Jana kulikua na mitanange tofauti-tofauti ya Europa katika madimba mbalimbali ya ulaya na kuwapa watu burudani ya soka.

Katika dimba la Old Trafford kulikuwa na furaha ya kutosha baada ya kugawa dozi kwa wageni wao waliowaalika kutoka nchini Ufaransa kwa kuwapa dozi ya kutwa mara tatu kwa bila.
Jijini manchester jana kulikua na mchezo kati ya Manchester United dhidi ya Saint Entienne ya nchini Ufaransa kwa kuwafunga goli tatu kwa bila magoli yakifungwa na mchezaji mmoja raia kutoka Sweden Zlatan Ibrahmovic(Abra-Cadabla)kwa kufunga dakika ya 14 na sekunde 27 kwa kupiga faulo yenye ujuzi kwa kupiga mpira wa chini uliowapita mabeki wa St Entienne na kuzama kwenye nyavu za wapinzani kunako dakika ya 74 na sekunde 29 katika kipindi cha pili alifunga goli la pili na kumaliza mchezo kwa kupiga penati iliyotokana na kufanyiwa madhambi ndani ya boksi kwenye dakika ya 86 sek 17 na kupiga mkwaju huo kwenye dakika ya 87 na sekunde 17 uliofunga pazia la magoli hayo matatu na kuondoka na gozi lake la ng"ombe.
Kwa upande wa kina Samatta Krc Genk ambao walikuwa wageni walitoka sare na Astra Giurgiu ya nchini Romania kwa kufungana magoli mawili kwa mawili katika mchezo huo wa piga nikupige.

Powered by Blogger.