MANCHESTER UNITED YAGAWA DOZI HADI UGENINI

Manchester United inazidi kupasua anga katika Europa ligi kwa kugawa dozi hadi Ugenini.

Klabu ya Manchester United ya nchini Uingereza wanazidi kupasua anga kwa kugawa dozi hadi Ugenini kwa kuichapa klabu ya St Etienne nyumbani kwao nchini Ufaransa katika kiota cha Geoffroy Guichard kwa kipigo cha goli moja kwa bila kutoka kwa kiungo wake Henrikh Mkhitaryan ndani ya dakika ya 15 akipokea pasi kutoka kwa mchezaji Juan Mata ingawa kiungo huyo aliyeshinda goli alipata majeruhi katika mtanange huo nakupelekea kutolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na kinda Marcus Rashford na mchezaji mwingine aliyeumia ni kiungo Michael Carrick nae nafasi yake kuchukuliwa na Bastian Shweinsteiger na kadi nyekundu kutolewa kwa beki wake Eric Bailly kuelekea hadi mwisho wa mchezo huo kumalizika kwenye ubao ukisomeka kwa goli moja kwa bila na kuwapa nafasi Manchester United ya kupasua anga  katika 16 bora ya Europa ligi na kuiondoa klabu hiyo ya nchini Ufaransa kwa jumla ya magoli 4-0.

.
Powered by Blogger.