MANCHESTER UNITED WANYANYUA KOMBE MBELE YA SOUTHAMPTON


Usiku wa jana Februari 26 ndio kulikua mtanange wa fainali ya EFL CUP 2017 kati ya Manchester United dhidi ya Southampton.

Manchester United imefanikiwa kupata ushindi wa goli 3-2 katika mchezo huo wa fainali, Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovich raia wa Sweden anaibuka kuwa shujaa wa Manchester United baada ya kufunga goli la ushindi alianza kufunga goli la kwanza ndani ya dakika 19 kuelekea dakika ya 39 Jesse Lingard akifunga goli la pili na kwenye dakika ya 87 yuleyule Zlatan Ibrahimovich anamalizia hesabu ya magoli kwa kufunga goli la tatu ambalo lililoipa ushindi Manchester United.
Licha ya Southampton kuonesha jitihada za kusaka ushindi na kufanikiwa kusawazisha goli mbili za mwanzo kupitia kwa Manolo Gabbiadini dakika ya 45 na 49 na kuutawala mchezo kwa asilimia 52 na Manchester United asilimia 48, haikusaidia Southampton kupata ushindi.Powered by Blogger.