MANCHESTER CITY WAPATA PIGO KWA MCHEZAJI WAO HUYU

Manchester City inaweza kupata pigo kwa kumaliza ligi kwa  kumkosa mshambuliaji wake wa muhimu kwa kuwa na majeruhi ya mguu.

Mchezaji huyo raia wa Brazil aliyetua manchester City msimu huu akitokea katika klabu ya Palmeiras ya nchini kwao Brazil amepata majanga katika mchezo wake wa pili walioshinda kwa goli mbili kwa bila dhidi ya Bournamouth siku ya jumatatu ndipo mguu wake wa upande wa kulia uliposhtuka katika dakika ya 15 na kupelekea kuteguka kitaalam wanaita(Metatarsal) na kutoka nje ya uwanja na nafasi yake kuchukuliwa na mshambuliaji mwenzake Sergio Aguero raia wa Argentina.
Kuteguka huko kumepelekea awekewe kiatu kigumu cha kunyooshea mfupa wa mguu.Majeruhi hayo yanaweza kumpelekea akawa nje ya uwanja kwa muda wa mrefu sana sawa na msimu mzima.
Powered by Blogger.