Luffa afunguka juu ya uhusiano wake yeye na Nahreel kwa sasa


Baada ya Nahreel kuondoka kwenye studio za Switch Records miaka miwili iliyopita na kwenda kuanzisha studio yake, The Industry, studio hiyo inayomilikiwa na Quick Rocka iliyumba. Pia uhusiano kati ya wawili hao uliharibika kwa muda.

Switch Records ilikuja kupata nguvu tena baada ya Luffa kushika usukani na kufanikiwa kutengeneza hits kadhaa ikiwemo ngoma mpya ya sasa ya Joh Makini, Waya.

Watu walitarajia kuwa Nahreel na Luffa wangekuwa maadui hasa kwakuwa tayari ameonekana kutumiwa na wasanii waliokuwa wakifanya kazi na The Industry wakiwemo Jux, Vanessa Mdee na Weusi.

 “Nahreel tumefahamiana baada ya mimi kusikika, tukawa tunakaa pamoja, tunashare idea hivyo na hivyo na mambo yanaenda,” Amesema Prod Luffa.
Powered by Blogger.