Licha Ya Ujauzito Alionao, Beyonce Atatumbuiza Kama Kawaida Kwenye Tamasha La Coachella

 
Baada ya Beyonce kutangaza kuwa ana ujauzito wa watoto mapacha wiki hii, mashabiki wake waliokuwa wameshanunua tiketi kwenye kumshuhudia kwenye tamasha la Coachella, waliingiwa na wasiwasi kuwa hatoweza kutumbuiza.

Hata hivyo kwa mujibu wa TMZ, show yake itafanyika kama kawaida, licha ya kuwa na viumbe wawili tumboni. Vyanzo vilivyo karibu na Bey, vimedai kuwa staa huyo hana mpango wa kusitisha show yake, na tayari ameshawabook wasanii wawili wakubwa kumpa kampani.

Wasanii hao imedaiwa kuwa wote walikuwa wanajua awali kuwa muimbaji huyo ni mjamzito. Mmoja wa watumbuizaji hao ni msanii wa Roc Nation.

Tamasha hilo litafanyika April 14-16.
Powered by Blogger.