Maskini Kylie Jenner, Utamuonea Huruma Kwa Haya Maamuzi Ya Mahakama


Kylie Jenner anatajwa kwenye orodha ya watoto wenye ushawishi mkubwa duniani,  Akiwa na umri wa miaka 19 tu mrembo huyu anaemnyima usingizi rapa Tyga tayari anatajwa kuwa na utajiri unaofikia dola milioni 10 za kimarekani.

Utajiri wake unatokana na mikataba anayochukua kutoka kwenye makampuni kadhaa ya vifaa mbalimbali hususan nguo na urembo pamoja na Brand yake ya "Kylie Cosmetics"

Hivi karibuni kulizuka mgogoro kati ya Kylie Jennner na mwanamuziki wa siku nyingi Kylie Minogue, mgogoro ambao uliwaweka wawili hao katika hali ya kutoelewana kwa kile kilichotajwa kugombea jina la "KYLIE" kama nembo ya biashara (Trademark).

Mwanamama Kylie Minogue ameshinda kesi hiyo kwa kuangalia vigezo kibao ikiwemo umri, Kylie Minogue amekaa kwenye game ya muziki kwa zaidi ya miaka 30 umri ambao Kylie Jenner mwenyewe hajaufikisha.

Kwa mantiki hiyo Kylie Jennner atatakiwa kubadilisha jina lake la biashara kutoka "Kylie Cosmetics" na liwe jina lolote ambalo yeye na timu yake wataamua.YOUNG MONEY INARUDI,MSIKIE DRAKE HAPA AKITHIBITISHA HILO:
 
Powered by Blogger.