Kigwangalla aahidi kutoa orodha ya mashoga

 
Mkuu wa mkoa Dar es salaam, Paul Makonda baada ya kupamba moto na suala la kupiga vita madawa ya kulevya, Naibu waziri wa Afya Dr. Hamisi Kigwangalla nae ameamua kutoa tamko juu ya katazo la mapenzi ya jinsia moja na kusimamia kidedea swala hilo kwani lipo  nje ya maadili ya Afrika na Tanzania kwa ujumla.

Kutokana na tabia iliyokithiri ya watu hao wanaosapoti mapenzi ya jinsia moja kutumia mitandao ya kijamii kujianika. Naibu waziri wa afya atoa tamko.

”Nikirudi Dar kabla ya kuhamia Dodoma nitaweka wazi orodha ya watuhumiwa wa ushoga wanaojiuza mitandaoni, kuna watu wanadhani vita dhidi ya ushoga ni ya mzaha, ni vita kubwa na tutaishinda, nitaendesha operesheni kamatakamata.” amesema Naibu Waziri Hamisi Kigwangalla.

Naibu Waziri, ameeleza uchunguzi dhidi ya watuhumiwa wa ushoga unaendelea, endapo mashoga hao watapatikana watakamatwa kimya kimya na kusaidia kutaja wenza wao.

”kuna nchi marafiki zinafanya jitihada kupenyeza ushoga Tanzania kudai haki ya binadamu kuchagua ampendaye, sisi tunasema NO ”. amesema kigwangalla.
Powered by Blogger.