Kama Haujaiona "Marry You" Ya Diamond Platnumz Na Neyo Basi Pitia Hapa


Kama tunavyomjua Baba wa Princess Tiffah na Prince Nillan hapa namzungumzia Baba watoto wa Zarina Hassan AKA Zarithebosslady mshikaji wa kuitwa Diamond Platnumz, kupuyanga kwake ni adimu, hajawahi kuwaangusha mashabiki wake tangu ajiingize kwenye game ya bongoflava,

Alianza kama masihara baada ya kuiachia "Kamwambie" moja kati ya ngoma ambaz
o zilisumbua sana mwaka 2009.

Wengi waliomsikia Diamond kwenye kamwambie walimtabiria makubwa mbongoflava huyo. Miaka imezidi kusonga tukiziona hustle zake mpaka leo vijana wengi wa kitanzania wanaishi maisha ya mshikaji.

Amekua mfano wa kuigwa kadri siku zinavyozidi kusonga anatoa hitsong kwa kila ngoma inayotoka. Ukiachana na Salome ambayo alifanya ndio Latest song ya Diamond Platnumz ipo Kokoro ya Rich Mavoko mmoja kati ya vichwa hatari kabisa kunako Record Label ya "WCB".
Kokoro imefanikiwa kufanya vizuri mwishoni mwa waka 2016, Huku akiendelea kuzishika headlines kwenye Bongoflava Diamond Platnumz ameenda mbali zaidi na kuanza kuziachia zile kolabo zake na wasanii wakubwa kama alivyoahidi nkufanya mambo makubwa zaidi mwaka huu 2017.

Utakua uliwahi kuisikia "Marry You" ambayo kwa mara ya kwanza Diamond na Neyo waliitambulisha kwa wapenda burudani wa jiji la Mwanza kupitia tamasha la "Jembeka Festival"

 Sasa unaambiwa video ya ngoma hiyo imeachiwa na tayari imeanza kuonekana kwenye baadhi ya vituo vikubwa vya TV ikiwemo "Trace Africa".

Kabla video halisi ya wimbo huo kuweko kwenye mtandao wa Youtube, @SeeTheAfricanTV imefanikiwa kudaka audi ya wimbo huo na tumeona sio mbaya kuishea na wewe.

Enjoy Nayo Hapa:

 
Powered by Blogger.